heri ya sikukuu

m ndo nilyehitimu chuo,bila kuijua TCU,
msomi wa chuo kikuu,naundisha watoto a,e,i,o,u
sina makuuu,maana serekeli yetu ina meno na mguu
usawa huu lazima hata mwenye wazazi atajifanya yatima,
ili apate kipoozeo cha sikukuu,..

utamu wa michano

chorus
HII MCHANO ZINANIPA RAHA………….UTAMU
RAHA………..UTAMU..
RAHA.UTAMU
HII  MICHANO ZINANIPA RAHA
RAHAAAAAAAAAAAAAA
RAAAAHHHHHHAAAAAAAAAAAAAA
UTAMU  UTAMU UTAMUU
UTAMUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

Verse 1
Jeeeaaaa
Hii michano ni michano  Tanganyika unganisha na Zanzibar,
Michano ya katiba mpya,ccm jumlisha chadema,
M nachana tu..mpaka  michano inaniambia endelea,
Potezea , mchele mchele wakanda miwa..wabana pua bania..hii ni order..
Piga hip hop  madj,punguzeni nidhamu ya uwaoga..
Changanya vorco na mashavu,elimu itambe madume yapunguze kutoga,
Sina sitakabazi na maisha,nasitakabazi na hizi flow,

Jongoo ,kiongozi wa bandaa la wagumu na mabisho,

sikukuu njema

nakula bata ndefu,mpaka tabata inageuka kwa mtogele,
kama upo poa ,tende sawa toa kitu weka kitu weta mpe dole,
haya maisha tu,kama nimekukosea sorry,
ni nafanya yangu na lete kilo ya mbuzi,mpaka wamasai waseme yelo subai,
subai,we arifu ni kwere sana ulibidi uishi dubai,
sata rumba ruka majuka,waga pombe na hakuna atakeleuliza,we lipuka,
na kula meza moja na mafisadi wa kuu,wakuu wa epa na mabosi wa ehura,
lati ningekuwa mbuge,leo hata adui yangu angenipa kura...


raaaahhhhhhhhhhhhhhaaaaaaaaaaaaa
sikuku njemaaa

salamu ya sikukuu

leo sikukuu,kitaa wali nazi,
chunga sana ,viduku kumwaga radhi,
kutana na yatima na wahitaji,
acha kutawanya pesa kwa wanyoyaji,
leo ndo leo kijiko ndani ya mfuko,
msuli mkubwa,tanga suti mwiko,
huku niliko,ni soda tu ,na juice za kopo,
kakando kando na milupo,kando kando na mikosho,
asante allaha,idd mubaraka ,ishalaaaaah,,,



ed njema wakubwaa...

du..

Pesa hazihitaji umbea ndo maana hazishindi kabisa saloon
Kitaa kimemsahau bodea ,jilieze wewe utabuna lin,
Masuper star na vimin,maana mapaja yameja mikunjo ,uso poda na makunyazi,
Hiki kizazi,baba na lala na mwana chumba kimoja,lini ataweza kumpa radhi,
Siku hizi mitahani inavuja nab ado mtahiniwa anapata zero,
Huu ni utani ,mwekezaji amafunga kuku kwenye ardhi ya mchele,
Gasi inavuka mipaka ,wamakonde wamefingwa kengele,
Mademu wa siku hisi poda nyingi ,mikogo asha ngedere,
Maproduza uswazi na mabeat fuju,mpaka wimbo unageuka makelele,
M superstar,niliyemuuwa ,mpaka young killer,
Kisa ni mrs superstar kumgombania kabula,
Pesa imeshasaula nguo,tatizo mimi mume bwege,
Pedege kwenye gongo,fukura klabu cha mbege.
M ndo muuza ngenge nisiye jua bei ya nyanya wala kitungu,

Msomi wa chuo kikuu,niliyehitumu bila kujui TCU,

(nitaendelea next time )
ukitaka nikutungie nyimbo piga simu tu 0713 592224 au 0767592224 mstari ya uhakika..

TATIZO NINI?

VERSE 1&2
Hivi kwa nini pesa yetu inashuka dhamani,
Kuna nini ,marekani,viongozi wetu jamani,
Hivi ni nani,Yule anayeshinda makanisani,
Sera  gani zinagawa,dhahabu zetu jamani,
Kuna nini mbona obama hakupita nyumbani,
Samaki wa magufuli watarudi lini jamani,
Nina zero ,Na hii necta itakubali nirudie mtihani,
Ricmond na epa hawa wana ndugu jamani,
Ni hii ya kagoda,majengo pacha ya nani,
M nawaza tu majibu nayakosa makini,
Hivi kwa nini secretary huwa avaa kimini,
Bosi anavaa soti,na haisi kumuita ofisi,
Kuwa nini posho hazija futwa bungeni,
Kuna nini Afya mbona dawa hazionekani mahospitalin,
Tembo wanaisha,mbugani hiv mlinz ni nani,
Twiga wetu walivyo ruka walitua kwa nani,
Hivi mbona hawarudi ,wamekwa njiani,
Nasikia nchi imeuzwa ,amenunua nani,
Ametoa tasilimu,au kakopa jaman,
Maisha ya ramani,atrasi kapewa nani,
Siutani,kaburu amefikaje mbugani,
Fisadi na pesa chafu,aziwaga makanisan,
Hivi kwa nini carolight haiishi sokoni,
Kiwanda chake kiko wapi,bongo au mamtoni,
Anasambaza nani,mbona hajulikani,
Pesa ya masikini haikai mfuko wa nyuma kwanini,
Yatima hadeki hivi sababu ni nini,
Haya maisha ni nini,mbona wengine wanalala chini,
Nasikia  mjini ni shule,mwalimu mkuu ni nani,
Wenye pesa wanaona masikini manyani,
Hivi hiyo pesa ni nini,labda itakuwa miwani,
Siku hizi bikira adimu uswahilinii,waziuza dukani,
Ingawa kuwa siri,haijulikani mnunuzi ni nani,
Nasikia huu mwaka wa shetani,ngoja nisubiri mwakani,
Nisubiri mwakani,umasikini wangu buriani,
Huku bomu huku sera sasa nichangue nani,
Siasa imeguuka jeshi,ina vikosi mpaka uwanjani,
Hivi kwa nini wenye pesa hawaogopi vyombo vya juu,
Mama,Mbona wenye pesa hatusomi nao chuo kuuu,
Warembo wa dar,kwa nini hawapatani na watembea kwa mguu,
Mbona kingereza kingi,unanitisha nisikutongoze we duu.
Kuvunga kwingi ukipewa nazi unavunja mpaka kifu,

Chorus
Hivi kwa nini haya yote yanatokea….
Ni kwa nini tunazidi potea,
Tatizo nini mbona  wakuu wanashindwa ongea..
Matatizo chungu zima,hakuna pa kuponea..  
(rudia mara mbili chorus)(verse ya 1 na 2 zimeonganishwa)

Huu wimbo ni mali halali ya USIKUMNENE BLOG….KWA mawasiliano piga simu 0713592224.)

WAMENICHOKOZA

Hawana verse, m nina verse zaidi yao,
M staa, mwanga namulika macho yao,
Haya maisha tu kada sikutaka kuwa hivi,
Master wa flow kali, kavu kavu bila beat,
Stata,sipandi dala dala usiweke siti,
M namiliki maisha, wana unamiliki ndoto,
Nina nyumba sinza,upo kwenu gongolamboto,
Unataka kubeto nani,utanikuta wapi kachaa,
M nashinda angani napaa, mwana unashinda net,
Unashinda net,kutwakucha  kutafuta mabint,
Damn,unajiita star huku mfukoni una kitambulisho,
Star wapi ,umiliki hata bito,star mchafu ,
Mguuni yebo yebo,          
Nasikia unajisifu jo,unabifu na mimi,
Eti tulikuwa wana nimekusaliti uamini,
Wewe ndo mwalimu wangu wa kuflow,
Wewe ndo unaenipa show,promota wangu  u no,
Shit,kibao juu yangu,beef na crew yangu,
Unachafua ,eti mwana mnazi balaa,
Hatujawahi hata onana,unanidi kachaa,
Unashangaa mwana sijui flow bado Napata show,
Wewe unajua flow,uajua show na bado unapata “O”
Traki zako ni soo,sinaishia magetton kariakoo,
Da eti na wewe msanii ,tunakutana kwenye msiba tu chale,
Mwana nakuona choko,unanunua bifu upate soko,
Unajisifu nachana kwa verse zako,beat lako,na nina flow kwa flow zako,
Dar inanijua kada,mni  simba, m ni ninja,
Choko ukikutana na mimi lazima ubebe kinga,
M ndo rapper wa kwanza kubadilisha maneno kwa vina,
Majina kwa jina,na samaki aliye hai kuchina,

Piga kimya ,kabla sijakuharibia wewe kima,

YAHAYA (MKE WA MTU)

Nasikia mke wa mtu ni digital,
Analogy hakina tena,
Mke wa mtu ni moto,huuotwi kwa mstari chunguza vyema,
Kaa chonjo kada nakupa tu tahadhari mapema,
Jana yahaya katembezwa uchi toka sinza mpaka ubungo mataa,
Watu wanashangaa,kweli mke wa mtu kazua balaa,
Mwanzo,Skendo zimevuja kita,jimama linatembea na jamaa,
Na jamaa,na jamaa ni mwana wangu balaa,
Yani Mwana tumekuwa wote kitaa,
Mwana mwenye ni yahaya muuza sukari guru,
Nikamvutia wanya yahaya,akagoma akataa,
Nakaona ,poa yawezekana,wanamsingizia kachaa,
Zikapita siku ,mwenzi ,mwaka yahaya hapatikani kitaa,
Kapigwa selo ya mapenzi,na jimama,mke wa mdosi wa kitaa,
Mke kageuga sugu,kamiliki jimbo kabisa kwa jamaa,
Akamnunulia nyumba na gari ya kutembelea kachaa,
Pesa haisihi mfukoni  yahaya akageuka bili geti wa mtaa,
Kweli ziki mwana haramu,leo pesa inamnenepesha kachaa,
Makeke yalizidi kitanda,yakamchanganya jimama balaa,
Maujuzi ya kitaa,zikamfanya mke wa mtu azidi mwange chapa,
Penzi likavuka mpaka wakaanza kufaya hadharani,
Taarifa zikafika mdosi,mkewe anatembea na fala mmoja mtaan,
Kikao cha dharula kikakaa,Mdosi akatoa silaha na chapa,
Pesa nyingi balaa milioni 200, atakaye mkamata  kachaa,
Msako ukanza kitaa,wakwanza mimi ,mawela ,ghetto wa kazagaa,
Wakanipigwa maswali yupo wapi kachaa,yupo wapi yahaya, nyoka,?
Mmoja akanishikia bastola kichwani, ile na guna akapiga moja hewani,
msako ukavuka sinza,mbezi,mpaka huko tegeta corner,
kila mtu anamsaka yahaya maana kashageuka  pesa,
yahaya wa sinza ,fala leo amegeuka pizza,ghafla
yahaya akaonekana vingunguti kwenye mabucha ya mbuzi,
wanaa  kumuona tu  wakapiga miluzi,
yahaya kuona so ikabidi ajisalimishe,
huu ndo ulikuwa mwisho wa muuza sukari guru,
leo anashinda majalalani yahaya kageuka kichaa,
mdosi kampiga sindano,nauoza taratibu kachaa,
kweli ni nimeamin mke wa mtu  ni balaaa,
ukitembea nae jiandae tu ipo siku utashangaa,
sure utashanga,majitu wanalishasema,
siku ya siku utakojoa dagaa,utachaa,kama yahaya alivyofubaa..

mwili nusu umeshaoza,anasubiria kufa kachaa..

SIRIKALI verse

Hizi verse siziuzi nazigawa bure,
Sirikali umeficha wapi,mkataba ule,
Pesa hakuna,dili hakuna ,sasa wapi tule,
Namuona obama,huku bush kwenye pori lile,
Maisha yametupiga ,kinywaji chetu gongo,
HukoARV inataka diet, muasirika  anashindia dongo,
Leo namwaga gesi,m mmakonde nishageuka mbongo,
Wanatuzulumu ,wanatumbandua wametugeuza gogo,
Hii ngoma zito,reli ya kati, dar es salaam ,kigoma,
Vigogo wameuza njia ,ili makontena  yasikose mzigo,
Hawa hawa Kutwa wako kwenye harambe,
 Wanaitwa vigogo,wanatulaza kwenye kiza kila siku mazee,
wakijiuzulu wamebaki huru,wako juu hawa maku…..
inaniuma sana,leo mmasai nakosa uhuru,
wapi nitalisha, pori zote zimamilikiwa na makaburu,
hee..makaburu wamepewa na maku…..,wamemikikisha ardhi yetu na uhuru,
Mungu wangu,nikikumbuka ya mbagala sitaki kabisa kuiona ges ikutua dar,
maana ilikuwa balaa ,miili mingine tuliikuta juu ya paa,
nashangaa dar ni bas lililoja,ingawa gesi inapata kiti hii ni balaa,
Haya majanga mpaka leo ,nchi ina ndege  mmoja,
Napata uwoga mpaka leo,nusu ya watu wanakula ugali bila mboga,
Maendeleo ya bongo pasua kichwa hakika,

Katikati ya nyumba mia za nyasi,kuna gorofa moja,

MWANAHAWA VERSE

Stop kwanza,umekaza ,na u mrembo wa kuliza,
Simama kwanza,samahani kwa kukukwaza,….
Nachana juu ya biti,juu yako malikia,
U mrembo,mtori inayonukia,
Hy whatsapp, mpaka  vibe nasikia,
Kwako ni chuma ulete, nichume nilete wote,malikia,
Maliza vyote,ben kwangu jikubali twende sote.
Kwangu we gesi ya mtwara mmakonde nimesha lala,
Mwandishi wa makala,ala za roho ninapolala,
Heshima,upendo, na huu urembo unanivunja taya,
Mikogo,vituko,kila nikikuona nakosa power,
Unanikosha mwanya ,kubali niwe wako mwanahawa,
Mdomo unatetemeka  inatamka : nakupenda kwa shida,
Maana kweli nimependa mpaka kuongea nashindwa,
Nashindwa mwezio kuvumilia,kila nikikuona naumia,
Natamani uwe wangu niwe wako wa maisha,
Uwe fb yangu, nikuperuzi kila dakika,
Hakika unakila kitu ninacho kitaka,
Special one,kwangu we ni special honey,
Kitu gani kubali ,kubali nikupele nyumbani,
Nyumbani kwa maninja,mchumba accept tudake ndinga,
Napenda unavyopenda vile ninavyo flow,
Vinavyo shambulia floor,Kada sitokuacha baby u no.
Natamani uwe wangu verse hii upige back vorco,
Tufanane  ugeuke necta,nigeuke morko,
Tujuane kama pusha na muuza gongo,
Napambana usiku kucha m nasaka bingo,
Nije kukutuza,wangu ini mkalia nyongo,

La zizi wa roho,kingasiti,mamayoyo,,,,