SIRIKALI verse

Hizi verse siziuzi nazigawa bure,
Sirikali umeficha wapi,mkataba ule,
Pesa hakuna,dili hakuna ,sasa wapi tule,
Namuona obama,huku bush kwenye pori lile,
Maisha yametupiga ,kinywaji chetu gongo,
HukoARV inataka diet, muasirika  anashindia dongo,
Leo namwaga gesi,m mmakonde nishageuka mbongo,
Wanatuzulumu ,wanatumbandua wametugeuza gogo,
Hii ngoma zito,reli ya kati, dar es salaam ,kigoma,
Vigogo wameuza njia ,ili makontena  yasikose mzigo,
Hawa hawa Kutwa wako kwenye harambe,
 Wanaitwa vigogo,wanatulaza kwenye kiza kila siku mazee,
wakijiuzulu wamebaki huru,wako juu hawa maku…..
inaniuma sana,leo mmasai nakosa uhuru,
wapi nitalisha, pori zote zimamilikiwa na makaburu,
hee..makaburu wamepewa na maku…..,wamemikikisha ardhi yetu na uhuru,
Mungu wangu,nikikumbuka ya mbagala sitaki kabisa kuiona ges ikutua dar,
maana ilikuwa balaa ,miili mingine tuliikuta juu ya paa,
nashangaa dar ni bas lililoja,ingawa gesi inapata kiti hii ni balaa,
Haya majanga mpaka leo ,nchi ina ndege  mmoja,
Napata uwoga mpaka leo,nusu ya watu wanakula ugali bila mboga,
Maendeleo ya bongo pasua kichwa hakika,

Katikati ya nyumba mia za nyasi,kuna gorofa moja,