TATIZO NINI?

VERSE 1&2
Hivi kwa nini pesa yetu inashuka dhamani,
Kuna nini ,marekani,viongozi wetu jamani,
Hivi ni nani,Yule anayeshinda makanisani,
Sera  gani zinagawa,dhahabu zetu jamani,
Kuna nini mbona obama hakupita nyumbani,
Samaki wa magufuli watarudi lini jamani,
Nina zero ,Na hii necta itakubali nirudie mtihani,
Ricmond na epa hawa wana ndugu jamani,
Ni hii ya kagoda,majengo pacha ya nani,
M nawaza tu majibu nayakosa makini,
Hivi kwa nini secretary huwa avaa kimini,
Bosi anavaa soti,na haisi kumuita ofisi,
Kuwa nini posho hazija futwa bungeni,
Kuna nini Afya mbona dawa hazionekani mahospitalin,
Tembo wanaisha,mbugani hiv mlinz ni nani,
Twiga wetu walivyo ruka walitua kwa nani,
Hivi mbona hawarudi ,wamekwa njiani,
Nasikia nchi imeuzwa ,amenunua nani,
Ametoa tasilimu,au kakopa jaman,
Maisha ya ramani,atrasi kapewa nani,
Siutani,kaburu amefikaje mbugani,
Fisadi na pesa chafu,aziwaga makanisan,
Hivi kwa nini carolight haiishi sokoni,
Kiwanda chake kiko wapi,bongo au mamtoni,
Anasambaza nani,mbona hajulikani,
Pesa ya masikini haikai mfuko wa nyuma kwanini,
Yatima hadeki hivi sababu ni nini,
Haya maisha ni nini,mbona wengine wanalala chini,
Nasikia  mjini ni shule,mwalimu mkuu ni nani,
Wenye pesa wanaona masikini manyani,
Hivi hiyo pesa ni nini,labda itakuwa miwani,
Siku hizi bikira adimu uswahilinii,waziuza dukani,
Ingawa kuwa siri,haijulikani mnunuzi ni nani,
Nasikia huu mwaka wa shetani,ngoja nisubiri mwakani,
Nisubiri mwakani,umasikini wangu buriani,
Huku bomu huku sera sasa nichangue nani,
Siasa imeguuka jeshi,ina vikosi mpaka uwanjani,
Hivi kwa nini wenye pesa hawaogopi vyombo vya juu,
Mama,Mbona wenye pesa hatusomi nao chuo kuuu,
Warembo wa dar,kwa nini hawapatani na watembea kwa mguu,
Mbona kingereza kingi,unanitisha nisikutongoze we duu.
Kuvunga kwingi ukipewa nazi unavunja mpaka kifu,

Chorus
Hivi kwa nini haya yote yanatokea….
Ni kwa nini tunazidi potea,
Tatizo nini mbona  wakuu wanashindwa ongea..
Matatizo chungu zima,hakuna pa kuponea..  
(rudia mara mbili chorus)(verse ya 1 na 2 zimeonganishwa)

Huu wimbo ni mali halali ya USIKUMNENE BLOG….KWA mawasiliano piga simu 0713592224.)