Hawana verse, m nina verse zaidi yao,
M staa, mwanga namulika macho yao,
Haya maisha tu kada sikutaka kuwa hivi,
Master wa flow kali, kavu kavu bila beat,
Stata,sipandi dala dala usiweke siti,
M namiliki maisha, wana unamiliki ndoto,
Nina nyumba sinza,upo kwenu gongolamboto,
Unataka kubeto nani,utanikuta wapi kachaa,
M nashinda angani napaa, mwana unashinda net,
Unashinda net,kutwakucha
kutafuta mabint,
Damn,unajiita star huku mfukoni una kitambulisho,
Star wapi ,umiliki hata bito,star mchafu ,
Mguuni yebo yebo,
Nasikia unajisifu jo,unabifu na mimi,
Eti tulikuwa wana nimekusaliti uamini,
Wewe ndo mwalimu wangu wa kuflow,
Wewe ndo unaenipa show,promota wangu u no,
Shit,kibao juu yangu,beef na crew yangu,
Unachafua ,eti mwana mnazi balaa,
Hatujawahi hata onana,unanidi kachaa,
Unashangaa mwana sijui flow bado Napata show,
Wewe unajua flow,uajua show na bado unapata “O”
Traki zako ni soo,sinaishia magetton kariakoo,
Da eti na wewe msanii ,tunakutana kwenye msiba tu chale,
Mwana nakuona choko,unanunua bifu upate soko,
Unajisifu nachana kwa verse zako,beat lako,na nina flow kwa
flow zako,
Dar inanijua kada,mni simba, m ni ninja,
Choko ukikutana na mimi lazima ubebe kinga,
M ndo rapper wa kwanza kubadilisha maneno kwa vina,
Majina kwa jina,na samaki aliye hai kuchina,
Piga kimya ,kabla sijakuharibia wewe kima,